Tovuti na mifumo salama · Zanzibar

Daftari linaandika.Mfumo unafanya kazi.

Ninajenga tovuti na mifumo salama inayochukua nafasi ya madaftari, Excel na kamisheni kubwa — kwa hoteli, migahawa, shule na SACCOS.

  • Bei za wazi
  • Dhamana siku 30
  • Domain na code ni zako
Picha ya Hamadi IddiUnaongea na anayejenga.Hamadi Iddi · BSc Computer Networking · msingi wa cybersecurity
Tatizo

Tatizo si kukosa juhudi. Ni zana zisizoendana na biashara yako.

  1. 01

    Oda za karatasi zinapotea, na wateja wanasubiri.

  2. 02

    Kila booking ya mtandaoni inapita kwa mtu wa kati na kamisheni yake.

  3. 03

    Stoo na mauzo vinahesabiwa kwa mkono mwisho wa siku.

  4. 04

    Tovuti ya zamani haifunguki vizuri kwenye simu, wala haina usalama.

Ninachojenga

Zana inayokosekana kwenye biashara yako.

Imejengwa kwa jinsi unavyofanya kazi, inajaribiwa na watakaoitumia, na ni mali yako.

Tovuti zinazouza

Kwa Kiswahili na Kiingereza, zinafunguka haraka kwenye simu, na zinaleta wateja moja kwa moja kupitia WhatsApp na Google.

Booking na malipo

Wageni wanabook na kulipa kwa M-Pesa au kadi moja kwa moja kwako, bila kamisheni ya mtu wa kati.

Mifumo ya ndani

POS, stoo, ada za shule, michango ya SACCOS — namba zako kwa wakati halisi, badala ya madaftari matano.

Mbinu

Mfumo wa K·J·K: hatua 3, na ushahidi 1.

  1. Kagua

    Ninaangalia jinsi biashara yako inavyofanya kazi leo, na gharama halisi ya njia ya sasa. Kisha tunaamua pamoja: tuendelee au tusiendelee.

  2. Jenga

    Michoro unayoikubali kwanza, kisha ujenzi. Unaona maendeleo kila wiki, na wafanyakazi wako wanaijaribu kabla ya kuzinduliwa.

  3. Kabidhi

    Mafunzo kwa timu yako, domain na code kwa jina lako, na dhamana ya siku 30.

  4. Pima

    Baada ya siku 60 tunapima matokeo pamoja: muda uliookolewa, oda, booking za moja kwa moja.

Kazi

Mifumo niliyojenga kwa matatizo halisi.

Jaribu demo ya oda kwa QR — kama mteja wako angeiona kwenye simu yake.

Taasisi isiyo ya kiserikali

Zanzibar Community Vision Foundation

Tovuti inayoeleza programu, maeneo ya kazi na timu, yenye njia za kuchangia, kujitolea na kushirikiana, pamoja na fomu ya mawasiliano na WhatsApp.

Ona ikiwa hewani
Migahawa

Mfumo wa Oda kwa QR

Mteja anascan QR mezani, anaagiza kwenye simu yake, na jikoni wanaona oda papo hapo kwenye dashboard.

Famasi na maduka

Mfumo wa Famasi

Mfumo wa stoo, mauzo na ankara wenye tahadhari za dawa zinazokaribia kuisha muda na ripoti za kila siku.

Taasisi

Mfumo wa Sampuli na Vifaa vya Maabara

Mfumo wa kusajili sampuli, kufuatilia vifaa na kutoa ripoti safi kwa uongozi.

Si kwa kila mtu.

  • Biashara yako inaendelea, lakini zana zako haziendani nayo.
  • Unapoteza saa nyingi kwenye kazi za mkono.
  • Uko tayari kuwekeza ili kujenga kitu cha kudumu.
  • Unatafuta bei ya chini kabisa.
  • Unataka template ya bure iliyobadilishwa rangi.
  • Huna muda wa kutoa picha na maelezo ya biashara.
Bei

Bei za wazi. Hakuna mshangao.

Bei kamili hutolewa baada ya mazungumzo ya bure, kulingana na mahitaji yako.

Msingi

Kwa biashara inayotaka kuonekana mtandaoni.

TSh 350k+

  • Wiki 1–2
  • Kurasa 3–5
  • Inafanya kazi vizuri kwenye simu
  • Fomu ya mawasiliano na kitufe cha WhatsApp
  • Ramani ya Google Maps
  • SSL (https) na usalama wa msingi
Uliza kuhusu Msingi

Biashara

Inayochaguliwa zaidi

Kwa hoteli, migahawa na biashara zinazopokea wateja mtandaoni.

TSh 800k+

  • Wiki 3–4
  • Hadi kurasa 10
  • Booking au orodha ya bidhaa
  • Blog au habari
  • SEO ya msingi ili upatikane Google
  • Lugha mbili: Kiswahili na Kiingereza
Uliza kuhusu Biashara

Mfumo maalum

Mfumo unaojengwa kwa jinsi biashara yako inavyofanya kazi.

TSh 2.5M+

  • Wiki 6+
  • POS, mauzo na stoo
  • Booking ya hoteli au mfumo wa shule
  • Malipo ya simu na kadi
  • Akaunti za wafanyakazi na ruhusa
  • Ripoti za kila siku
Uliza kuhusu Mfumo maalum

Hosting na domain

TSh 30,000 – 60,000 / mwezi

Tovuti inakaa hewani, na email ya biashara kwenye domain yako.

Matengenezo

TSh 50,000 – 150,000 / mwezi

Masasisho, backup, ufuatiliaji wa usalama na saa 2 za mabadiliko kila mwezi.

Msaada wa mfumo

TSh 150,000 – 400,000 / mwezi

Kwa mifumo maalum: msaada wa watumiaji, marekebisho na maboresho madogo.

Matengenezo kuanzia TSh 50,000 kwa mwezi · Malipo: 50% kuanza, 50% kabla ya kwenda hewani.

Hatua ya kwanza

Kabla ya kila mradi: ukaguzi wa bure.

Bure · dakika 2 kujaza · hakuna masharti.

  1. 1Usalama na kasi ya tovuti yako ya sasa
  2. 2Kazi zipi zinakula muda wako zaidi
  3. 3Gharama halisi ya njia ya sasa
Anza ukaguzi wangu

Nakagua tovuti ambazo mwombaji ni mmiliki au ana ruhusa ya mmiliki tu.

Maswali

Unayojiuliza.

Domain na tovuti vitakuwa mali ya nani?

Wewe. Domain inasajiliwa kwa jina la biashara yako, na unapata access zote mara malipo yanapokamilika.

Malipo yanafanyikaje?

50% kabla ya kuanza na 50% kabla ya tovuti kwenda hewani. Kwa mifumo mikubwa tunaweza kugawanya malipo kwa awamu tatu. Unaweza kulipa kwa simu au benki.

Inachukua muda gani?

Kifurushi cha Msingi ni wiki 1–2, Biashara wiki 3–4, na mifumo maalum kuanzia wiki 6. Muda unategemea pia jinsi picha na maandishi yanavyopatikana haraka.

Tayari nina tovuti. Unaweza kuiboresha?

Ndiyo. Tunaanza na ukaguzi wa bure wa usalama na kasi, kisha nakupa mapendekezo na bei ya kuiboresha au kuijenga upya.

Nini kikiharibika baada ya kuzindua?

Dhamana ya siku 30 inashughulikia hitilafu bila malipo. Baada ya hapo, mpango wa matengenezo unakupa backup, masasisho ya usalama na msaada.

Unatumia WordPress?

Inategemea. Tovuti za kawaida zinaweza kutumia WordPress ili uweze kubadilisha maudhui mwenyewe; mifumo maalum inajengwa kwa code ili iwe salama na ifanye kazi kama biashara yako inavyohitaji.

  1. 01 · Wewe
  2. 02 · Biashara
  3. 03 · Muda

Tujuane kwanza.

Ninajibu ndani ya siku 1 ya kazi. Taarifa zako hazitumwi kwa mtu mwingine.